Genesis 5:12-25

12 aKenani alipokuwa ameishi miaka sabini, akamzaa Mahalaleli. 13Baada ya kumzaa Mahalaleli, Kenani aliishi miaka 840, akawa na watoto wengine wa kiume na wa kike. 14Kenani aliishi jumla ya miaka 910, ndipo akafa.

15Mahalaleli alipokuwa ameishi miaka sitini na mitano, akamzaa Yaredi. 16Baada ya kumzaa Yaredi, Mahalaleli aliishi miaka 830, akawa na watoto wengine wa kiume na wa kike. 17Mahalaleli aliishi jumla ya miaka 895, ndipo akafa.

18 bYaredi alipokuwa ameishi miaka 162, akamzaa Enoki. 19Baada ya kumzaa Enoki, Yaredi aliishi miaka 800, naye akawa na watoto wengine wa kiume na wa kike. 20Yaredi aliishi jumla ya miaka 962, ndipo akafa.

21 cEnoki alipokuwa ameishi miaka sitini na mitano, akamzaa Methusela. 22 dBaada ya kumzaa Methusela, Enoki alitembea na Mungu miaka 300, na akawa na watoto wengine wa kiume na wa kike. 23Enoki aliishi jumla ya miaka 365. 24 eEnoki akatembea na Mungu, kisha akatoweka, kwa sababu Mungu alimchukua.

25 fMethusela alipokuwa ameishi miaka 187, akamzaa Lameki.
Copyright information for SwhNEN